Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwaisabula: Musonda bado Yanga

Kennedy Musonda Jr Mwaisabula: Musonda bado Yanga

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Kenny Mwaisabula, amemfuatilia kwa kina mshambuliaji mpya wa Yanga, Kennedy Musonda raia wa Zambia, katika michezo aliyoichezea timu hiyo na kusema "bado ana kazi kubwa ya 'kukopu' mfumo wa timu hiyo" kwa kuwa muda ni mdogo kuweza kuwa sawa.

Yanga ilimsajili Musonda katika usajili wa dirisha dogo uliofungwa Januari 15, mwaka huu kwa lengo la kusaidiana na kinara wa mabao wa timu hiyo, Fiston Mayele, ili kuleta ushindani katika Ligi Kuu Bara na mechi za Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga inayoiwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, itashuku dimbani ugenini nchini Tunisia Jumapili wiki hii kuwavaa wenyeji wao, Us Monastir katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi.

Akizungumza na Nipashe jana, Mwaisabula alisema kuwa, mara nyingi usajili wa dirisha dogo wachezaji wamekuwa na ugumu kidogo kuweza kwenda na mfumo tofauti na dirisha kubwa, hivyo itampa wakati mgumu Musonda kuweza kuelewana na Mayele kwa haraka.

"Musonda anaweza kusaidiana na Mayele, lakini dirisha dogo wachezaji 'kukopu' inachukua muda kidogo tofauti na dirisha kubwa watu wanakuwa katika kipindi cha preseason hivyo  wanajiandaa na timu tofauti na sasa.

"Mchezaji kukopu anachukua muda, inakuwa rahisi kwa mchezaji ambaye amecheza ligi hii kama vile Saido (Ntibazonkiza), imekuwa rahisi kutokana na kuijua ligi ya hapa tofauti na mchezaji kutoka nje ya ligi hii," alisema na kuongeza:

"Mchezaji kutoka nje pia itamchukua muda kuweza kumzoea mwalimu, wachezaji na hata mazingira aliyoyakuta, hivyo itamchukua muda kidogo Musonda kwenda sawa na Mayele."

Aidha, akizungumzia kuhusu Bernard Morrison kuwa nje kwa miezi miwili kutokana na majeruhi ya nyonga, hivyo kushindwa kuichezea Yanga mechi za kimataifa, Mwaisabula alisema:

"Litakuwa ni pengo kukosekana kwa Morrison katika michuano ya kimataifa kwa kuwa ni mchezaji wa kimataifa na ana uzoefu wa mechi za kimataifa hivyo angeisaidia timu.

"Lakini naamini Yanga itafanya vizuri kwa kuwa ina wachezaji wazuri wa kimataifa kama Aziz Ki na Mayele."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: