Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yanyesha mashabiki wakomaa kwenye foleni

Mashabiki Yanga Shangwe Mashabiki wa Yanga

Sun, 28 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya uwepo wa mvua Wananchi wameamua kukomaa kwenye foleni za kuingia uwanjani mapema kulishuhudia chama lao la Yanga likicheza fainali ya kwanza dhidi ya USM Alger kwenye uwanja wa Mkapa.

Wananchi wanaonekana kuitika huku utaratibu wa kuingia uwanjani ukiwa ule ule kama ambavyo imekuwa katika michezo kadhaa iliyopita.

Huku wakisimamiwa na watu wa usalama, shabiki mmoja baada ya mwingine wamekuwa wakipita kwenye vizuizi kwa ajili ya zoezi la kuhakiki ticketi zao kisha kuingia uwanjani.

Nyuso za mashabiki hao zinaonekana kubeba matumaini ya timu yao kufanya vizuri kwenye mchezo huo. Hakuna matumizi yoyote ya mabavu ambayo yanaonekana kutumiwa na watu wa usalama, Wananchi wanaonekana kufuata vizuri taratibu elekezi.

Wakati wengine wakiingia uwanjani wapo ambao wanazurura nje huku wengi wao wakitafuta ticketi licha ya kutangazwa zimemalizika tangu jana.

Vikundi mbalimbali vya ushangiliaji navyo vinalimsha nje ya uwanja huu ikiwa ni sehemu ya hamasa.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: