Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mutale amekuja na familia yake mazima

Dsv Joshua Mutale Mutale amekuja na familia yake mazima

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambiuliaji wa Power Dynamos ya Zambia, Joshua Mutale ametua nchini kusaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu ya Simba kwa msimu ujao .

Mutale ametua jana usiku nchini akiwa na familia yake kwa ajili ya kukamilisha dili lake na Simba ambayo wanaonesha dhamira ya kuinasa saini ya nyota huyo mwenye uwezo wa kucheza winga wa kulia.

Imeelezwa ujio wa nyota huyo nchini ni baada ya mazungumzo pande zote mbili kwenda vizuri na muda wowote kuanzia sasa atasaini mkataba wa miaka mitatu kutumikia timu hiyo kwa msimu ujao.

“Mazungumzo yalifanyika mapema pande hizo mbili na ujio wa Mutale hapa nchini ni kukamilisha taratibu zingine ikiwemo kusaini mkataba makubalino ni miaka mitatu kuitumikia klabu hiyo,” amesema Chanzo hicho.

Meneja wa Idara ya habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema usajili unaendelea kufanyia na baadhi ya wachezaji wapya tayari wameshasaini mkataba na kuitumikia Simba msimu unaokuja.

Amesema kwa sasa zoezi lililopo ni kuwaongezea mkataba wachezaji walimaliza na kutakiwa kuendelea kusalia katika kikosi cha timu hiyo kwa kuanza na Mzamiru Yassin, Israil Mwenda na Kibu Denis.

“Usajili wa nyota wapya unaendelea tunaleta watu. Waliomaliza mkataba tunaemtaka atabaki tu akihitaji tumpe dunia nzima ili abaki Simba tutampa kwa maslahi ya klabu, kifupi ni kuwa hatushindwani na mahitaji ya mchezaji,” amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: