Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musonda awahidi furaha Wananchi

Yanga Skudu Aucho Musonda.png Musonda awahidi furaha Wananchi

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Mzambia, Kennedy Musonda amesema kuwa yeye na wachezaji wenzake wapo fiti na tayari kuwavaa wapinzani wao Al Merrikh ya nchini Sudan.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Jumamosi (Septemba 16) kwenye Uwanja wa Kigali Pele ulio katika Mji wa Kigali, Rwanda ambako utapigwa mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Musonda amesema kuwa maandalizi aliyoyafanya yanatosha kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo, kuelekea mchezo dhidi ya Al Merrikh.

Musonda amesema kuwa wanahitaji ushindi dhidi ya Al Merrikh watakaokuwa nyumbani ili kuwaongezea presha wapinzani wao, watakaporudiana jini Dar.

“Kama mchezaji nipo tayari na fiti asilimia mia moja kucheza mchezo dhidi ya Al Merrikh, ni mchezo ambao tunahitaji kupata ushindi kwa lengo la kuwapa furaha mashabiki wetu.

“Kikubwa nilichopanga ni kutumia vema kila nafasi nitakayokuwa ninaipata katika mchezo huo kwa kufunga mabao na kuwatengenezea wachezaji wenzangu. “Ninaamini mchezo utakuwa mgumu, lakini nitahakikisha ninaipambania timu yangu, kama nikipata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza,” amesema Musonda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: