Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musonda atabiriwa makubwa Yanga

Kennedy Musonda Man Of The Game Kennedy Musonda.

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans wala hauna presha licha kuondoka Mshambu ya wao tegemeo, Fiston Kalala Mayele, kwani umeweka wazi kuwa mshambuliaji wao Kennedy Musonda anaweza kuwa mfungaji bora wa msimu ujao na atavunja rekodi kibao za washambuliaji waliopita.

Musonda kwa sasa ndiye Mshambuliaji tegemeo ndani ya Young Africans mara baada ya Mayele kuuzwa huku pia wakimshusha Hafizi Konkoni raia wa Ghana kama mbadala wake jambo ambalo mashabiki wengi wamekuwa na hofu kubwa.

Akizungumza jijini Dar es salaam Ally Kamwe ambaye ni Afisa Habari wa Young Africans amesema kuwa: “Watu wanamuona Musonda kama ni mshambuliaji wakawaida sana lakini mimi niwaaambie kuwa yule mtu anajua sana kufunga na anajua sana mpira na msimu ujao watamtambua.

“Niwahakikishie kuwa yule mshambulaiji atakwenda kuvunja rekodi zote za washambuliaji ambao wamewahi kucheza kwenye hii ligi, watu wanaona kama utani lakini mimi namshuhudia, kiu yake ya kutaka kufanikiwa zaidi na Young Africans na malengo yake ni makubwa mno.

“Sisi wala hatuna presha na Young Africans ya msimu ujao ukiona kuna mtu anaondoka, basi fahamu huyo ambaye anakuja ni moto wa kuotea mbali kuliko hata yule ambaye ameondoka,” amesema kiongozi huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: