Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musonda akabidhiwa mikoba ya Mayele Yanga

Insta Mayele Musonda Musonda na Mayele.

Fri, 21 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Yanga, Kennedy Musinda amekabidhiwa rasmi mikoba ya aliyekuwa mshambuliaji kinara wa timu hiyo, Fiston Mayele kuelekea mechi ya siku ya Kilele cha Wiki ya Mwananchi itakayopigwa kesho katika Dimba la Mkapa.

Hilo limesemwa na Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe wakati akizungumza na chombo kimoja cha habari kuelekea mchezo huo wa kesho ambapo yanga watakipiga na Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini ambao mpaka sasa wameshatua kwenye ardhi ya Tanzania.

"Watu wote waliohudhuria mazoezi wanasema pale Avic Town wanasema mpira unaanzia kwa Diarra, kila mmoja anaugusa mpaka kwa Kennedy Musonda anaweka ndani.

"Sasa tunataka tuwaonyeshe watu kwamba baada ya kumalizana na Kaizer Chiefs tutakutana naoo Tanga na mechi za msimu ujao. Kaizer atakuwa kipimo chetu na ujumbe utafika kwa wengine," amesema Kamwe.

Kwa kauli hiyo inaonyesha dhahiri kuwa huenda, Mayele asiwepo kesho na si sehemu tena ya kikosi cha Yanga msimu ujao, baada ya tetesi kuwa amesajiliwa na Pyramids FC ya nchini Misri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: