Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musonda aapa kuwaua Waarabu

Kennedy Musonda First Goal Musonda

Fri, 17 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Yanga, Kennedy Musonda ameapa kuhakikisha anafunga mabao muhimu yatakayoisaidia timu yake kufanya vizuri dhidi ya US Monastir.

Musonda ambaye ni ingizo jipya kwa Yanga mpaka sasa amefanikiwa kuifungia timu hiyo bao moja katika Kombe la Shirikisho Afrika ambalo alifunga dhidi ya TP Mazembe.

Akizungumza nasi, Mshambuliaji huyo alisema kuwa: “Binafsi natamani kuona naisaidia Yanga kwa kufunga mabao muhimu katika mchezo wetu dhidi ya US Monastir, najua ni ngumu lakini nitajitahidi.

“Nilipofunga dhidi ya TP Mazembe nilijisikia vizuri, nilifahamu ulikuwa ni mchezo mgumu na muhimu kwetu Yanga, hivyo nilihisi kuwa niliwafurahisha sana Wanayanga.

“Hata katika mchezo wetu huu muhimu dhidi ya Monastir natamani kufunga ili niendelee kuwafurahisha Wanayanga na wazidi kuwa na imani na mimi, muhimu ni wao kuja kwa wingi uwanjani,” alisema mchezaji huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: