Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mudathir atamba na rekodi CAF

Mudathir Yahaya Abbas Yes Mudathir atamba na rekodi CAF

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga, Mudhathir Yahya, ameweka rekodi yake kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuwa mzawa pekee aliyefunga hatua ya makundi.

Yanga ikiwa imetinga robo fainali ya michuano hiyo, ni mabao 8 wamefunga, huku 7 yakifungwa na wachezaji wakigeni kwenye msako wa ushindi.

Mudhathir alipachika bao hilo kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao uliposoma Yanga 3-1 TP Mazembe akitumia pasi ya Kennedy Musonda raia wa Zambia.

Sio ndani ya Yanga tu, hata kwa watani zao wa jadi Simba inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika hakuna mchezaji mzawa ambaye ametupia bao hatua ya makundi licha ya timu hiyo kufunga mabao 9.

Yanga kinara wao wa utupiaji ni Fiston Mayele mwenye mabao matatu, yeye ni raia wa DR Congo, Mzambia Kennedy Musonda (2), Jesus Moloko (1) na Tuisila Kisinda (1) wote raia wa DR Congo.

Ndani ya Simba ambayo imetinga robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika, mabao yote yamefungwa na wageni ambapo kinara ni Clatous Chama mwenye mabao manne, huyu ni raia wa Zambia, Hennock Inonga wa DR Congo (1), Jean Baleke kutoka DR Congo (2) na Sadio Kanoute raia wa Mali (2).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: