Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mudathir anavyompa usalama Khalid Aucho

Mudathiir X Khalid Auchoo Mudathir anavyompa usalama Khalid Aucho

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimu ukiwa unaanza kila mchezaji anatakiwa kuangalia nini alikifanya msimu uliopita kama kilikuwa kibaya anahitaji maboresho.

Sadio Kanoute aliongoza kwa kuwa na kadi nyingi za njano (10), kuliko mchezaji yeyote hivyo msimu huu anaweza kuzipunguza kama ataamua, lakini kwa upande wa Khalid Aucho ndiye mchezaji aliyeongoza kwa kadi za njano ndani ya Yanga SC akionyeshwa mara (4).

Hadi sasa amecheza michezo yote miwili ya Ligi Kuu na hajaoneshwa kadi huku Yanga ikishinda michezo yote kwa jumla ya mabao 10.

Kuna sababu nyingi ambazo zinamfanya Aucho awe sehemu salama miongoni mwa hizo ni pamoja na uwepo wa Mudathir Yahya kwenye eneo la katikati.

Mudathir amekuwa na kiwango kikubwa sana msimu huu, ukiuangalia mchezo dhidi ya JKT Tanzania, mchezaji huyo alifanya kazi iliyomweka Aucho sehemu salama.

Aucho hakusumbuliwa sana na wapinzani kwenye eneo lake kwa kuwa Mudathir alizunguka kila sehemu ya hatari, alikuwa kama rada, mchezaji gani wa Yanga angependa Mudathir kuwa nje ya uwanja?

Hakika huyu ni mchezaji ambaye hata Azam FC leo hii wakimuangalia kuna sehemu viongozi wanajikosoa wenyewe, hatari sana kuiacha silaha kama hiyo ikaenda upande wa pili.

Aucho sasa atakuwa na amani kucheza na Mudathir, Aziz Ki pia angetamani kumuona Mudathir akiwa naye uwanjani kwa dakika zote kwa kuwa anaonekana kuupenda mpira na kuipenda Yanga SC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: