Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mudathir: Yanga ina wachezaji bora kuliko Simba

Mudathir Yahaya Abbas Yes Mudathir Yahya

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya Abbas amesema timu yao kwa sasa ina wachezaji bora wa kuamua mchezo wa ‘Kariakoo Derby’.

Akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa habari, Mudathir alisema wanawaheshimu Simba lakini sisi Yanga tuna wachezaji wazuri kuliko wao wenye uwezo wa kuiamua mechi.

“Mchezo tunaamini utakua mgumu. Sisi hatuidharau Simba lakini ukitazama kikosi chetu, tuna wachezaji wengi wazuri kuliko wao wenye uwezo mkubwa wa kuiamua mechi.

“Niwaombe mashabiki wetu kuja kwa wingi Benjamin Mkapa siku ya kesho na sisi tutapambana kuhakikisha tunawapa furaha,” alisema Mudathir

Kesho Yanga tutashuka dimba la Mkapa kucheza dhidi ya watani wetu, Simba SC kwenye mchezo wa mzunguko wa 26 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: