Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mudathir Yahya anavyoutaka uadmin katika Group la Viungo wa Soka nchini

Mudathir Yahya.jpeg Kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Tanzania yote ipo Kizimkazi ambapo Rais Samia amezindua miradi kadhaa ya Maendeleo, basi kuna Kiungo wa mpira mbali na Kizimkazi anafanya kazi ya kuwapa wakazi wa Chamazi burudani ya bei rahisi, anakaba kuliko Vibaka wa Keko, anafunga kuliko Hakimu na nyundo Keko na anapiga pass kuliko Dobi.

Haitwi Rasta kama Kibu D, haimbwi kama Msanii Chibu D, ila katikati ya Kipaji ongeza bidii, alipolichukua dimba baada ya Faila Suu kuondoka akasema sit back and enjoy greatness! Kabla ya Shuu ya Nassib wa Tandale alikuwa anapiga pass za Waiter leta pale na mtelezo kama Kambale wa maporomoko ya Hale.

Mitaa inatamja Ustadh Aucho wa ardhi ya Kaguta Museven, ila kalamu na mbao za mbinu pale Avic Town zinasema There is only one Mudathir, ni Andrea Pirlo wa bei rahisi! Ni TRA ya Yanga Afrika, ni Bodi ya Mikopo ya Viungo wote na kama Chuo cha soka basi yeye ndio TCU, kama mpira wa Yanga ni computer basi yeye ni CPU, certified Premier League Baller.

Chid wa Ilala alisema Dar Es Saalaam Stand Up, Gigy alisema Kiki ni Gigy, Michael Jackson alisema Man in the mirror basi leo tuondoke na hii kuwa Mudathir ndio Yanga ya Dar, ndio Kiki ya tano tano na ndio Mwanaume kwenye kioo nyuma ya soka la Wananchi.

Mudathir Yahya anautaka Uadmn Group la Viungo wote,

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: