Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mudathir, Farid wafunga na rekodi yao CAF

Faridi Muda Mudathir na Farid

Thu, 6 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kupata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans van der Pluijm amefunguka kuwa wapo tayari kupambania ubingwa wa michuano hiyo.

Mchezo huo ulipigwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Liti uliopo mkoani Singida ambapo mabao ya Singida yaliwekwa kambani na Bruno Gomes aliyetupia mabao mawili, Francis Kazadi na Bright Adjei.

Akizungumza nasi, Pluijm alifunguka: “Matunda yetu ya kambi tuliyofanyia Dodoma kwa ajili ya mchezo huu yameonekana kwa sababu kwa mara ya kwanza mwaka huu tumefunga mabao mengi zaidi.

“Sasa tumeingia rasmi hatua ya nusu fainali na ikishafika hatua hii basi lazima uwe tayari kukutana na mpinzani yeyote, sisi kwa upande wetu tupo tayari kupambania ubingwa wa michuano hii.

“Wachezaji wangu wanazidi kuimarika, morali yao inazidi kuongezeka, wanafuata kile ninachowafundisha ndiyo maana mpaka hivi sasa tumepata mafanikio makubwa ikiwa ni msimu wetu wa kwanza katika Ligi Kuu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: