Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msimu wa maokoto kwa Azizi KI, ashindwe yeye tu

Aziz Ki Goli Bora Stephen Aziz KI

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwisho wa msimu huu mkataba wa Aziz KI na Yanga utafikia tamati wakati ambao mashabiki wa Yanga wameshaanza kuvutiwa na mvinyo wake ambao ameendelea kuwakwekea kwenye glasi zao.

Hakuna namna kwa ubora alionao anayeweza kuthubutu kutamka kwamba fundi huyo wa mguu wa kushoto aondoke kama ambavyo waliondoka mastaa wengine Djuma Shaban au Mamadou Doumbia.

Utamu wa Aziz KI utakuwa shubiri mezani au kete muhimu atakapokutana na uongozi wa Yanga kujadili hatua ya kuurefusha mkataba wake.

Katika majadiliano hayo nyota huyo hatatumia nguvu kubwa kwani ataweka maneno kidogo kisha akiwaacha wakubwa kufikiria kwa hesabu ndefu akijua tayari alishapanda mbegu sahihi kwa kiwango chake anachoendelea kuonyesha hivi sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: