Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshery arejea mazoezini Yanga

Mshery Mshery arejea mazoezini Yanga.

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa Yanga SC, Aboutwalib Hamad Mshery aliyekuwa nje kwa majeraha amesharejea kiwanjani kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Kipa huyo alikuwa na majeraha ya goti na majeraha hayo yalimfanya awe nje kwa nusu msimu uliomalizika.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram kipa huyo ameonyesha picha yuko katika uwanja wa mazoezi wa timu hiyo, Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Urejeo wa Mshery ndani ya kikosi hicho unakifanya kikosi hicho kiwe na makipa watatu, Djigui Diarra, Metacha Mnata na Mshery.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: