Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshery aomba kuondoka Yanga

Mshery  1024x1024 Abou-Twalib Mshery

Fri, 7 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuitumikia Yanga kwa misimu mitatu ya mafanikio kipa namba mbili wa timu hiyo nyuma ya Diarra Djigui, kipa Abuutwalib Mshery imedaiwa ameomba kuondoka kusaka timu ambayo itampa nafasi ya kucheza ili kujihakikishia namba timu ya taifa, Taifa Stars.

Mshery alijiunga na Yanga, Desemba 2021 hivyo ameitumikia timu hiyo kwa misimu mitatu yenye mafanikio kwa kutwaa mataji ya Ligi Kuu na Kombe la FA huku akiwa miongoni mwa wachezaji walioifikisha timu hiyo kucheza fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo cha kuaminika kutoka kwa rafiki yake wa karibu wa kipa huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na timu ya taifa ya vijana ya Serengeti Boys, kililiambia Mwanaspoti kuwa, Mshery amemaliza mkataba ndani ya Yanga na mpango wake ni kupata timu itakayompa nafasi ya kucheza mara kwa mara ili aweze kupata nafasi ya kuitumikia Taifa Stars.

“Mshery alisaini mkataba wa miaka mitatu ambayo tayari imeisha mwisho wa msimu huu sasa yupo timu ya taifa mambo yake ya kusaini mkataba timu nyingine bado hayajafanyika ila mpango wake ni kupata timu ambayo itamuakikishia nafasi ya kucheza,” kilisema chanzo hicho.

Mwanaspoti lilifanya juhudi za kumtafuta Mshery, ili kujua ukweli wa jambo hilio naye alikiri kweli mkataba wake na Yanga umeisha, lakini aligoma kuweka wazi ofa alizozipata hadi sasa ikiweka wazi kuwa muda ukifika kilakitu kitawekwa wazi.

“Ni kweli nimemaliza mkataba na Yanga baada ya msimu huu kuisha na nafurahi kuwa na misimu mitatu bora ndani ya timu hiyo licha ya changamoto mbalimbali nilizokutana nazo ikiwa ni pamoja na kukaa nje ya uwanja kwa muda kutokana na kusumbuliwa na majeraha,” alisema Mshery na kuongeza;

“Nipo kwenye kambi ya timu ya taifa nilikuwa na misimu bora ndani ya Yanga ni muda wa kulitumikia taifa mambo ya mkataba mpya kila mmoja atafahamu sio suala la mimi kulizungumzia kuna watu wananisimamia hiyo ndio kazi yao.” Alisema.

Kuisha kwa mkataba wa Mshery kunamfanya aungane na Metacha Mnata ambaye pia mkataba wa mkopo wa miezi sitaaliokuwa nayo kuitumikia timu hiyo akitokea Singida Fountaine Gate umemalizika, hivyo sasa kuifanya Yanga iwe imesaliwa na Diarra tu na yule wa kipa was timu ya vijana U20 na kuupa kazi uongozi kuongeza nguvu kwenye timu hiyo ambayo imetwaa mataji ya ligi matatu na Kombe la FA mfululizo.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: