Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrithi wa Onyango kimeeleweka Simba

Che Fondoh Malone Che Fondoh Malone

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa zinasema kuwa Simba imeanza mazungumzo rasmi na Klabu ya Cotton Sports ya Cameroon kwa ajili ya kumsajili beki wa kati wa timu hiyo, Che Fondoh Malone ambaye anatajwa kuwa mrithi wa beki, Joash Onyango ambaye amewasilisha barua ya kutaka kuondoka kikosini hapo.

Hiyo ni katika kuelekea usajili wadirisha kubwa litakalofunguliwa hivi karibuni wakati Ligi Kuu Bara imemalizika. Simba tayari imeanza kufanya usajili wa kikosi chake, ikiwa imemsajili tayari mshambuliaji wa Rayon Sports ya Rwanda, Willy Onana.

Taarifa ambazo tumezipata, tayari mazungumzo kati ya uongozi wa Simba na wasimamizi wa mchezaji huyo, Royal Soccer Management yameanza kwa ajili ya kumsajili.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa upo uwezekano wa beki huyo kujiunga na Simba kutokana na menejimenti ya mchezaji huyo kugomea baadhi ya ofa kadhaa ambazo wamepelekewa mezani.

Aliongeza kuwa kama mazungumzo yakienda vizuri, basi beki huyo atatua nchini hivi karibuni kwa ajili ya kukamilisha dili hilo la mkataba wa miaka miwili.

“Katika dirisha la usajili la mwezi Januari baadhi ya klabu zilionyesha nia ya kumuhitaji Malone, lakini yeye mwenyewe amegomea na kusimamia msimamo ya kuja kuichezea Simba.

“Hivi sasa mazungumzo yanakwenda vizuri, hivyo muda wowote atatua nchini kwa ajili ya kukamilisha dili la usajili katika kuelekea dirisha kubwa la usajili,” alisema mtoa taarifa huyo.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa timu wa Simba, Ahmed Ally akizungumzia masuala ya usajili ya timu hiyo, alisema: “Mazungumzo yanakwenda vizuri na baadhi ya wachezaji, mara baada ya usajili huo kukamilika kila kitu tutaweka wazi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: