Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrithi wa Manula Simba vitani na Baleke

Ally Salim Gh Mrithi wa Manula Simba vitani na Baleke

Wed, 3 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinda mlango wa Simba, Ally Salim anayetajwa kuwa mrithi wa Aishi Manula kutokana na uwezo mkubwa anaouonyesha ndani ya timu hiyo kwa sasa, ametajwa kuingia fainali ya kinyang’anyiro cha kumsaka mchezaji bora wa mashabiki wa timu hiyo kwa mwezi Aprili.

Katika hatua hiyo Salim ambaye amekuwa gumzo baada ya kuziba pengo la Manula aliye na majeraha ya bega anatarajiwa kuchuana na mastaa wengine wawili wa timu hiyo ambao ni mshambuliaji wa kimataifa wa DR Congo, Jean Baleke na kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Kibu Denis.

Ndani ya mwezi Aprili, Salim amefanikiwa kuichezea Simba michezo miwili ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu na Yanga na michezo miwili ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya Robo Fainali dhidi ya Wydad Casablanca huku akifanikiwa kupata clean sheet tatu na kufungwa bao moja pekee.

Baleke ndani ya mwezi Aprili amecheza mechi nne na kufunga mabao sita, huku Kibu akicheza michezo minne na kufunga bao moja na kuasisti mara tatu.

Akizungumzia tuzo hiyo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema: “Katika mwezi Aprili tumecheza mechi tano huku nyota hao wakionyesha kiwango bora na kuwa na takwimu nzuri. Zoezi la kupiga kura linatarajiwa kufungwa rasmi Mei 2, mwaka huu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: