Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moses Phiri: Nina deni kwa Mashabiki

Phiri Arudi Fiti Moses Phiri

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kitendo kilichofanywa na mashabiki wa Simba cha kupaza sauti kumtaka Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ampe nafasi kubwa ya kucheza Moses Phiri kimemfanya mshambuliaji huyo kukiri ana deni kubwa, huku akikiri kitendo hicho kimemuongezea nguvu na kuahidi kuwapa furaha.

“Mashabiki wana upendo mkubwa sana kwangu, jambo linalonifanya nipate nguvu ya kupambana kuhakikisha nafanya zaidi ya kile wanachokitarajia kutoka kwangu, ingawa siwezi kusema msimu huu nataka kufunga mabao mangapi, ila nitafunga kwa kadri ninavyoweza,” alisema Phiri na kuongeza;

“Ushindani ni mkali kwenye timu, ambao ni mzuri kwa kila mchezaji kuongeza bidii, ndio maana nani aanze kucheza na nani aanzie benchi kocha ndiye atakayeamua kulingana anavyoona mchezo husika.”

Phiri alisema yupo fiti kupambana kuhakikisha ligi inayoendelea anaonyesha ushindani kuanzia kwenye kikosi hadi timu pinzani na anashukuru nafasi anayopewa na makocha wa kikosi hicho na wajibu wake ni kutowaangusha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: