Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morrison aongeza mzuka Yanga SC

Morrison  Yangaaaaaa Morrison

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa kurejea uwanjani kwa winga wao, Bernard Morrison kutaongeza kitu ndani ya timu hiyo kuelekea katika michezo mingine migumu iliyopo mbele yao.

Morrison kwa mara ya kwanza amerejea kuitumikia Yanga katika mchezo wa juzi dhidi ya Geita Gold, mara baada ya kukaa nje kwa miezi miwili ambapo mara ya mwisho kuicheza Yanga ilikuwa katika mchezo ambao Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Azam FC.

Akizungumza nasi, Kaze alisema kuwa kitendo cha Morrison kurejea ndani ya Yanga na kuichezea timu hiyo kitakwenda kuwaongezea nguvu katika michezo yao migumu iliyopo mbele yao.

“Tunakwenda katika ratiba ngumu zaidi katika mwezi huu michezo migumu mbele yetu, mchezo wa dabi na ile ya kimataifa, hivyo tunahitaji kuwa na wachezaji wengi tena wenye uwezo mkubwa wa kuisaidia timu.

“Morrison amerejea na hii ni faida kubwa sana kwetu kwa kuwa kila mtu anafahamu uwezo wa Morrison, ni mchezaji mzuri hivyo tunaamini kuwa atatuongezea kitu katika michezo yetu hiyo ijayo ambayo ni muhimu kwetu kuwa na wachezaji wote wazima,” alisema kocha huyo.

Miongoni mwa mechi ambazo Yanga wanatarajia kuzicheza ni ile ya ligi kuu dhidi ya Simba na ile dhidi ya Rivers United ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: