Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moloko apewe heshima yake Yanga

Moloko Er Moloko apewe heshima yake Yanga

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jesus Ducapel Moloko ni mchezaji ambaye hapewi heshima na sifa inayomstahili kwenye soka la Bongo.

Anachukuliwa poa sana lakini mchango wake kwenye mafanikio ya Yanga ni mkubwa kuliko wachezaji wengi vipenzi vya Gongowazi.

Kuna wakati Kisinda alikuwa anathaminika na kuheshimika Gongowazi kuliko Moloko, wakati mchango wa Moloko kimbinu ni mkubwa kwa mbali kuliko Kisinda.

Haimbwi sana wala usajili wake haukuwa wa mbwembwe kama Aziz Ki, Musonda na wengine, hana makuu kiwanjani lakini anafanya mambo muhimu sana.

Mtengezaji mzuri wa nafasi na inapobidi kufunga. Nabi amemfanya kuwa silaha yake kimbinu na mara nyingi amemtumia kwenye miichezo migumu muhimu na mikubwa na hajamuangusha.

Anaweza asiwe Mayele, Bangala au Musonda, lakini ni zaidi ya Aziz Ki kwa mbali sana wakiwa kiwanjani kutekeleza majukumu ya kimbinu.

Anachokifanya kingekuwa kinafanywa na Morrison au Aziz Ki kingethaminika maradufu kwakuwa ni vipenzi vya wanajangwani.

Kuna wakati unahitaji winga halisi mwenye mwendo anaeweza kuwalaza hoi mabeki kisha anatengeneza nafasi, hapo unamtaka Moloko.

Unataka winga anaeweza kutumia nafasi nyuma na mabeki mbele ya kipa wa wapinzani akatengeneza nafasi ya kufunga, hapo unamtaka Moloko.

Hata Simba wangekuwa na winga wa aina hii wangepata ziada ya mbinu, Okra alijaribu ameishia njiani. Watanzania kuna aina yetu ya mpira ambao Moloko hatupi huo ndio maana haimbwi, ila yeye anafaa sana kwenye soka la kileo.

NB: Nabi ni kocha msikivu sana akiambiwa tatizo analifanyia kazi. Hongera kocha Nabi benchi la ufundi na wachezaji kwa kuingia robo fainali. Dunia imeshindwa kuzuia kifo na kuuficha ukweli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: