Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moloko akinukisha kambini Yanga

Moloko Drs Moloko akinukisha kambini Yanga

Tue, 28 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mkongomani, Jesus Moloko, amesema kuwa bado hawajamaliza, kwani wanazihitaji pointi za wapinzani wao, TP Mazembe katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, Yanga iliifunga TP Mazembe mabao 3-1. Kwa sasa Yanga imefuzu robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku TP Mazembe ikishindwa kufuzu. Zinakwenda kukamilisha ratiba kunako Kundi D.

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana Juni 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa TP Mazembe ambao upo kwenye Mji wa Lubumbashi nchini DR Congo.

Akizungumza nasi, Moloko alisema kuwa bado wana uhitaji wa pointi tatu kutoka kwa TP Mazembe ili walimalize kundi wakiwa bado kileleni ambapo kwa sasa wana pointi 10.

Moloko alisema kuwa watahakikisha wanaipeperusha vema bendera ya Yanga kwa kuhakikisha wanapambana na kufanikisha malengo ya kuongoza kundi.

Aliongeza kuwa, wachezaji pekee hawatatosha kupambana uwanjani, hivyo wanahitaji sapoti ya mashabiki watakaoungana nao katika safari hiyo ya Lubumbashi.

“Wachezaji pekee hatutatosha kufanikisha malengo ya timu kupata ushindi bila ya kuwepo mashabiki uwanjani, hivyo sapoti kubwa inahitajika siku hiyo tutakaporudiana na TP Mazembe.

“TP Mazembe wakiwa nyumbani wana sapoti kubwa ya mashabiki, hiyo ndio siri kubwa kwao ya ushindi, hivyo mashabiki wetu wa Yanga nao wanahitajika kuwepo kwa wingi siku hiyo uwanjani kwa ajili ya kutuongezea hamasa na hali ya kupambana.

“Sisi kama wachezaji tutatimiza majukumu yetu ya uwanjani ya kufunga na kucheza soka safi kwa ajili ya kuwapa furaha mashabiki wetu,” alisema Moloko ambaye hivi sasa yupo katika kiwango bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: