Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Dewji aweka pesa kumng'oa Mwamnyeto Yanga

Mwamnyetoo Znd Mo Dewji aweka pesa kumng'oa Mwamnyeto Yanga

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Inaelezwa kwamba Viongozi wa Simba wameanza kumnyapia beki wa Yanga Bakari Mwamnyeto baada ya kutokuwa na uhakika wa kuendelea kukipiga katika klabu hiyo.

Taarifa za uhakika zinaeleza kwamba Mwamnyeto bado hajaanza mazungumzo na Uongozi wa Yanga kuhusu kumuongeza mkataba mwingine.

Beki huyo wa Kati ambaye kabla ya kujiunga na Yanga mwaka 2022, alikuwa anahitajika zaidi na Simba lakini Mnyama alizidiwa ujanja na mchezaji huyo akasajiliwa upande wa pili.

Kwa msimu ulioisha Mwamnyeto alikuwa na ingia toka nyigi sana kwenye kikosi cha Miguel Gamondi, huku kocha huyo akionekana kuwapa nafasi zaidi Dickson Job na Ibrahim Bacca tofauti na ilivyokuwa enzi za Nasradinne nabi.

Kauli ya mchezaji huyo wakati wa kukabidhiwa kombe la ubingwa wa NBC alisema kwamba;

“Tusubiri msimu uishe tutaongea zaidi kuhusu hatma yangu Yanga, lakini mimi bado ni mchezaji wa Yanga na malengo ni kuchukua ubingwa wa FA” Aliongea Mwamnyeto.

Simba ndiyo klabu pekee inayohusishwa sana na kuhitaji saini ya mchezaji huyo, huku wakiwa tayari wamemsajili Lameck Lawi, na kumaucha Kennedy Juma na Henock Inonga naye yuko mbioni kuondoka.

Mchakato wa Simba kumsajili Bakari Mwamnyeto utategemea na hatma ya Beki wake Henock Inonga endapo atapewa Thank You, lakini kwa habari za kunyapia nyapia inaelezwa mchezaji huyo aliomba msamaha kwa kile alichokifanya ndani ya klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: