Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Dewji awapongeza Yanga "Wamefanya kazi kubwa"

Mo Dewji Mkapa Mo Dewji

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' amesema bado ndoto yake kubwa ni kuiona Simba ikitwaa taji la ligi ya mabingwa barani Afrika

Mo ambaye tangu aanze kuwekeza Simba, katika kipindi chake cha miaka mitano, Simba imefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya CAF mara nne

Simba imecheza robo fainali ya ligi ya mabingwa mara tatu na kombe la Shirikisho mara moja

Mo amesema Simba tayari ina mataji 22 ya ligi kuu, hivyo angependa zaidi kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa

Aidha Mo ameeleza kufurahia na ushindani ulioletwa na Yanga kwenye ligi ya ndani akiamini hiyo ni chachu kwao kujiimarisha na kuifanya ligi kuwa bora zaidi

"Nawapongeza Yanga kuleta ushindani mkubwa ndani ya Ligi wamefanya kazi kubwa, mpira usipokuwa na ushindani hauna ladha kwa hilo lazma niwapongeze Yanga na nawatakia kila La kheri kwenye mashindano Confederation na wao pia wafanikiwe ili timu nne ziendelee kushiriki kwenye mashinda haya makubwa"

"Mimi naona sisi (Simba) lazima tujipange upya ili tuweze sio tu kwenye Ligi. Huku kwenye ligi tumeshashinda mara 22 kwangu ni muhimu zaidi kushinda Champions League Africa," alisema Mo katika mahojiano na Global TV Online.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: