Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mnyama anamfuata Power Dynamos

Image 186.png Mnyama anamfuata Power Dynamos

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: Dar24

Kikosi cha Simba SC kimeanza safari ya kuelekea nchini Zambia tayari kwa mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa kuwania Kufuzu Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika 2023/24.

Simba SC itacheza dhidi ya Power Dynamos Jumamosi (Septemba 16) katika Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola Zambia.

Kwa mujibu wa kurasa za Mitandao ya Kijamii za Simba SC zimeonesha baadhi ya wachezaji wa Simba SC wakiwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es salaam, kabla ya kuanza safari ya kuelekea Zambia.

Mshindi wa jumla wa mchezo huo atatinga Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu 2023/24.

Chanzo: Dar24
Related Articles: