Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mmoroco kumuweka benchi Ally Salim Zambia

Ally Salim X Lakred Mmoroco kumuweka benchi Ally Salim Zambia

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba inatarajiwa kuvaana na Power Dynamos ya Zambia katika mechi ya mkondo wa kwanza itakayopigwa kesho kutwa Jumamosi, huku benchi la ufundi la timu hiyo likipanga kufanya sapraizi itakayowapa matokeo bora ugenini kabla ya kurudiana jijini Dar es Salaam.

Moja ya sapraizi ni badiliko kwenye eneo la kipa, benchi likipanga kumtumia Ayoub Lakred badala ya Ally Salim, huku mastaa wengine kama Saido na Henock Inonga wakiwa kwenye hatihati ya kuanzia benchini kwenye pambano hilo.

Lakred amesajiliwa na Simba kutoka FAR Rabat ya Morocco ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo ili kuziba pengo la Aishi Manula aliyeumia, lakini alikosa mechi mbili za Ligi Kuu.

Hata hivyo, wakati wa mechi hizo alikuwa kikosini akijifua na kupata uzoefu sambamba na kujenga maelewano bora na wenzake na kwa mujibu wa kocha wa makipa wa Simba, Lakred yuko tayari kwa mchezo na watu watarajie kumuona kikosini Zambia.

“Eneo la kipa ni nyeti sana, hauwezi kufanya mabadiliko bila ya tathimini ya kina. Lakred ni kipa mzuri na anafanya vizuri mazoezini, hapo mwanzo tulimpa muda ili azoee na kuelewana vyema na wenzake lakini kwa sasa yupo tayari kwa mchezo na ataonekana uwanjani,” alisema Cadena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: