Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkutano Mkuu Yanga 2023 anatambulishwa Staa gani?

IMG 4417.jpeg Wanachama wa Yanga wakiwa Ukumbini

Sat, 24 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Klabu ya Yanga leo Juni 24, 2023 imeitisha Mkutano Mkuu wa mwaka wa Klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo wa Klabu ya Yanga unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Daes Salaam.

Mbali na ajenda mbalimbali zitakazojadiliwa katika Mkutano huo kiu na hamu ya Mashabiki na wapenzi wa Klabu ya Yanga ni kujua Mkutano huo utamtambulisha staa gani.

Kwani kumbukumbu zinaonesha Julai 9, 2022 katika mkutano Mkuu wa Klabu mbali na uchaguzi uliofanyika wa viongozi lakini alitambulishwa staa aliekipiga EPL katika klabu ya Newcastle Gael Bigirimana kujiunga na Yanga.

Safari hii kiu na hamu ni kuona Staa gani atatambulishwa kurithi jezi namba 6 iliyokuwa ikivaliwa na Feisal Salum alietimkia Azam FC.

Je, unadhani ni nan atatambulishwa leo! Bashiri

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: