Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkude hawezi kuziba pengo la Bangala - Mchambuzi

Mkude Bangala Mkude hawezi kuziba pengo la Bangala - Mchambuzi

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Alex Ngeleza amesema kuwa kiungo mpya wa Yanga Sc, Jonas Mkude hataweza kuziba pengo la Yanick bangala ambaye ametimkia Azam FC.

Ngereza kupitia TV3 amedai kuwa, bangala ana uzoefu wa mashindano makubwa na na ana uwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji na kama beki wa kati hivyo kuondoka kwake Yanga ni hasara kubwa.

"Itakuwa ngumu kwa Jonas Mkude kuziba pengo la Yannick Bangala kwa sababu Bangala anakupa faida ya kutumika kwenye maeneo mawili tofauti kama beki wa kati na kiungo lakini Mkude anaenda kutumika kwenye eneo moja tu la kiungo.

"Sehemu nyingine ambayo itaenda kuathirika baada ya kuondoka Bangala ni eneo la beki wa kati, Yanga bado hawana beki wa kati mwenye uzoefu mkubwa kama Bangala ndio maana kuna baadhi ya mechi Nasridine Nabi alikuwa anamuweka kama beki wa kati kutokana na makosa ambayo walikuwa wanafanya mabeki wengine.

"Kwa hali jinsi ilivyo Yanga msimu ujao inaweza ikawa na safu mbaya ya ulinzi kama Gift Fred hataweza kuendana na mfumo wa mwalimu haraka kwa sababu hawana kina Nondo, Job na Bacca wamekuwa na changamoto nyingi kwenye safu ya ulinzi ndio maana asipokuwepo Bangala walikuwa wanafungwa magoli marahisi sana," amesema Alex Ngeleza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: