Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miquissone afunika utambulisho Simba, apewa namba ya Banda

Jose Luis Miquissone JJ.jpeg Miquissone afunika utambulisho Simba, apewa namba ya Banda

Sun, 6 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo Mshambuliaji wa Simba, Luis Miquissone amepokelewa kwa shangwe na mashabiki wa Simba waliojitokeza kwa wingi kwa Mkapa baada ya kutambulishwa wa mwisho kwenye kikosi cha timu hiyo chenye wachezaji 30.

Kiungo huyo ambaye aliitumikia kwa mafanikio Simba kabla ya kutimkia nje kwenda kujaribu changamoto nyingine amerudi na kupokelewa kwa shangwe akikabidhiwa jezi namba 11 iliyokuwa inavaliwa na Peter Banda ambaye amepewa namba 40.

Mbali na Miquissone ambaye amepokelewa kwa shangwe kubwa pia kipa namba moja wa timu hiyo Aishi Manula ambaye ameingia na binti yake amepokewa kwa shangwe sambamba na Mzamiru Yassin.

Huku kiungo Fabrice Ngoma akipewa jezi namba sita iliyokuwa inavaliwa na Pascal Wawa, Saidoo Ntibazonkiza amepewa jezi namba 10 iliyoanchwa na Peter Banda, Willy Onana amepewa jezi namba saba ambayo mara ya mwisho alivaa Chriss Mugalu.

Wakati Hamis Abdallah kapewa jezi ya Hamis Ndemla, David Kameta kapewa jezi namba tatu ya Gadiel Michael, Shaban Chilunda jezi namba 27 na Hamis Kazi kapewa namba ya mkongwe Erasto Nyoni 16.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: