Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miquissone, Onana wasikiliziwa

Jose Luis Miquissone Noma.jpeg Jose Luis Miquissone

Sun, 6 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Luis Miquissone ni miongoni mwa wachezaji ambao wanazungumzwa na mashabiki wa Simba kwenye tamasha la Simba Day huku wakidai kama amerudi na makali yake basi hakuna timu ya kuwazuia msimu wa 2023/24.

Mashabiki mbalimbali wa Simba wamekuwa katika mijadala ya hapa na pale wakati wakiendelea kuburudika katika tamashala lao la 15 tangu kuanzishwa kwake 2009.

Mmoja wa mashabiki hao, Juma Jafari ambaye amesafiri kutoka Mwanza, amesema tangu kuondoka kwa Konde Boy (Luis) hakuna mchezaji ambaye aliziba pengo lake.

Hivyo urejeo wake ni habari mbaya kwa wapinzani wao, Yanga maana wanajua vile mbavyo amekuwa moto wa kuotea mbali.

"Ni kama.kipepeo vile ndiye mchezaji ambaye amenifanya kusafiri kutoka Mwanza, namini amerudi na makali yake, ataanza kutupa raha kuanzia leo," amesema shabiki hiyo.

Aliyekuwa pembeni na shabiki huyo, alidakia kwa kusema Luis atakuwa amerudi kama alivyoondoka wanaweza kuzima kelele za mashabiki wa Yanga ambao wanasumbua.

"Kipindi fulani tulipoteza ubora wetu kwa sababu ya kuondokewa na baadhi ya wachezaji ndio hao wakiwa Luis na Chama, ninafurahia urejeo wao, acha sasa tuone moto wao tena," amesema.

Mbali na Luis ambaye alikuwa Al Ahly ya Misri mchezaji mwingine aliyesajiliwa kipindi hiki cha usajili anayetajwa uwanjani hapa ni Willy Onana.

Onana amesajiliwa kutoka Rayon Sports ya Rwanda ambapo msimu uliopita ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini humo (MVP).

Msimu uliopita Onana aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu nchini Rwanda baada ya kufunga mabao 16 na kusaidia kupatikana kwa mengine matano (asisti).

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: