Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda: Chama hatukupanga acheze dhidi ya Namungo

Chama Na Mgunda Mgunda: Chama hatukupanga acheze dhidi ya Namungo

Thu, 4 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amesema kuwa kiwango walichokionyesha wachezaji wa Simba katika mchezo wa jana dhidi ya Namungo wamekiona na watakwenda kukifanyia kazi huku akiwasihi mashabiki wa klabu hiyo kuwavumilia wakati benchi la ufundi likifanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo huo.

Mgunda amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kutamatika huku Simba akitoa sare ya bao 1-1 na Namungo katika Dimba la Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

Robertinho alipanga wachezaji saba wa kikosi cha pili huku ikiwapumzisha nyota wake kadhaa wakiwemo Chsama, Tshabalala, Inonga, Kapombe, Mzamiru, Kibu Denis na Kanoute.

“Wachezaji Tumewapa nafasi ya kuitumikia klabu, tulichokiona ni cha kwetu, na mwenye macho yake ameona, hivyo tulichokusudia kukiona na Robertinho tumekiona, tutaenda kufanyia kazi mapungufu kwenye mechi zilizosalia.

“Chama tumekuja naye na yupo lakini hakuanza, tumecheza na hatukuwa pungufu, kwa hiyo wachezaji wale ni wa Simba na ni haki yao kuitumikia klabu yao. Kila mmoja anapopata nafasi anatimiza wajibu wake.

“Kungekuwa na matatizo tungesema, Chama yupo na mazoezi amefanya, leo hajacheza ni sehemu tu ya mpangilio wa kazi, ilikuwa ni sehemu ya wengine kutimiza wajibu wao.

“Tuwaheshimu wachezaji wetu wakipewa nafasi ya kuitumikia Simba, ni haki yao. Na hawa ndio wachezaji wetu tuliosajili Simba, kwa hiyo tuwe na imani nao,” amesema Mgunda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: