Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu 'mwanzo mwisho' Kipa mpya wa Simba SC

IMG 4973.jpeg CV ya kipa mpya wa Simba ni hii

Sun, 23 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Leo Simba imemtambulisha kipa kutoka Brazil Luis Jefferson ikimsainisha mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo hadi mwaka 2025.

Kipa huyu mwenye umri wa miaka 29, jina lake ni Jefferson Luis Szerban de Oliveira Junior ana urefu wa mita 1.9 na kabla ya kujiunga na Simba alikuwa akiitumikia Resende FC ambayo inashiriki Ligi Daraja la nne, Brazil.

Hata hivyo, tangu aliposajiliwa na Resende mwaka 2017 muda mwingi alikuwa akitolewa kwa mkopo kwenda timu mbalimbali hadi kufikia hatua ya kutua Simba.

Luis ametolewa kwa mkopo kwenye jumla ya timu tano tofauti ambazo alikuwa kwa nusu msimu ama msimu mmoja pekee.

Timu hizo tano ambazo fundi huyu alipelekwa kucheza kwa mkopo ni pamoja na Athletic, Itabaiana, Volta Redonda, SC Aymores na Itabirito FC-MG.

Kwa msimu uliopita akiwa na Resende, kipa huyu amecheza mechi 21 za michuano yote akaruhusu mabao 35 na akamaliza mechi tatu bila ya nyavu zake kutikisika.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: