Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mexime: Tunajiandaa kuwakabili Yanga

Mecky Mexime Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime.

Thu, 6 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime aipigia hesabu kali Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Aprili 11 kuhakikisha anaibuka na alama tatu.

Kagera Sugar ipo nafasi ya saba ya msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 32 ambapo inatarajia kuvaana na Yanga Aprili 11 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza nasi, Mexime amesema kuwa, kikosi chake kipo vyema hivyo anajipanga kuikabili Yanga Aprili 11 ili kuweza kutwaa pointi tatu.

"Mchezo wetu unaofuata tunacheza na Yanga, siku zimeshakwisha hakuna muda wa kupumzika, tunahitaji kujiandaa ili kuweza kufanikiwa kutwaa alama tatu.

"Ligi ni ngumu na ina ushindani mkubwa hasa mechi hizi za mwisho kila timu inapambana kupata matokeo hivyo tunajipanga kuweza kupata matokeo mazuri," alisema Mexime.

Aidha, alimalizia kwa kusema kuwa, kikosi chake kipo vizuri hivyo wanajipanga kumaliza vizuri.

Ligi Kuu Bara ipo ukingoni ambapo kila timu imebakiza michezo mitano ili kukamilisha msimu wa 2022/23.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: