Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi kufanya maamuzi magumu

Messi Best FIFA Lionel Messi

Thu, 1 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lionel Messi anatarajiwa kufanya maamuzi muda mfupi ujao kuhusu wapi atacheza msimu ujao kitu pekee kinachoonekana wazi ni kwamba haitakuwa #Barcelona.

Messi angependelea kurejea mahali palipokuwa nyumbani kwake tangu alipoondoka Argentina akiwa na umri wa miaka 12 kwa ajili ya kutimiza ndoto yake ya soka.

Lakini kambi yake imeiambia Barcelona uamuzi juu ya mustakabali wake uko karibu kufanyika na hawawezi kusubiri tena ofa kutoka kwao ambayo haijawasilishwa mpaka sasa, licha ya ahadi kuwa klabu hiyo ya Catalan ingefanya hivyo kufikia sasa.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwenye umri wa miaka 35 anataka kusalia Ulaya lakini, baada ya kuamuliwa kuondoka Paris St-Germain msimu huu wa joto, ofa zinazokuja kutoka bara hilo hazivutii vya kutosha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: