Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meneja wa Mwanyeto: Ofa ya Simba iko mezani na ni nono

Mwamnyetoo Znd Bakari Mwamnyeto.

Tue, 25 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa wa Nahodha wa Klabu ya Yanga, Bakari Mwamnyeto aitwaye Carlos Sylivester amesema kuwa wamepokea ofa ya Klabu ya Simba kutaka huduma ya mchezaji huyo.

Simba wanatajwa kuitaka huduma ya Mwamnyeto kama mbadala wa Henock Inonga Baka ambaye ametimkia AS FAR Rabat ya nchini Morocco.

“Hakuna kinachokwamisha, ni suala la muda tu, muda sahihi ukifika tutajua mustakabali. Kwa sasa mazungumzo yanaendelea vizuri na sioni kitu cha kukwamisha lakini suala la kusema tumemalizana na Yanga bado.

“Unapoongelea ofa za hizi timu mbili, kitu ambacho Simba ana ofa sidhani kama Yanga anaweza kushindwa ku-ofa ama anachoweza ku-ofa Yanga basi Simba nae anaweza ku-ofa. Kikubwa ni uatayari wa mchezaji anataka kwenda kufanya wapi kazi.

“Maongezi yanaendelea vizuri lakini kwa mtu kama Mwamnyeto ni beki mzuri, ni nahodha wa yanga na amecheza kwa mafanikio makubwa ndani ya klabu, hajapata changamoto ambayo klabu haimhitaji, kwa hiyo maamuzi yanaweza kuchukua muda kwa sababu lazima ufikirie suala la kubadilisha mazingira.

“Pia ofa ambazo zinakuja na suala la uongozi wa mchezaji kukutana na uongozi wa timu, hicho ndicho kitu ambacho kimeleta tofauti lakini mazungumzo yako sawa. “Ni kweli ofay a Simba ipo mezani na ni nzuri pia, lazima tuitafakari pia. Ni suala la muda kama nilivyosema, muda utazungumza,” amesema Carlos.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: