Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meneja: Yanga wakimpata Sudi! watamsahau Mayele

Sudi Abdallah Player Mchezaji Sudi Abdallah anaetajwa kuja kuchukua nafasi ya Mayele

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga wakiumiza kichwa kumsaka mrithi wa Mshambuliaji wao Fiston Mayele anaetajwa kutimkia Uarabuni.

Miongoni mwa majina yanayotajwa ni Mshambuliaji Sudi Abdallah ambae ni mchezaji huru baada ya kuachana na Kuching City ya Malaysia.

Sasa Meneja wa mchezaji huyo ametoa neno kuhusiana na uwezo wa mchezaji huyo akisema;

“Uwezo wake wa kupambana uwanjani ni mkubwa sana bila kusahau mbinu na uzoefu alionao ndio uliowavutia zaidi Yanga, hivyo umri sio kikwazo.

Yanga hawatajutia kuwa naye, sisemi kwa sababu ni meneja wake ila kizuri kinajiuza nina uhakika atafanya makubwa.”

Je Wananchi mko tayari kumpokea Sudi Abdallah Mitaa ya Jangwani?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: