Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mdau: Kuala Lumpa Malaysia, waleee nusu fainali!

Mayele Yanga Riversss Mdau: Kuala Lumpa Malaysia, waleee nusu fainali!

Mon, 1 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuala Lumpa Malaysia Umoja wa Mataifa, Waleeeeeeee nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Wino wa dhahabu umeshawekwa katika vitabu vya kihistoria, sio kazi rahisi na kila mmoja ndani ya nafsi yake anakiri hilo sio lazima aseme hadharani.

Yanga ilikuwa timu ya kwanza ya Tanzania kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika tangu muundo wa mashindano hayo ulipobadilika mwaka 1997 na imekuwa timu ya kwanza ya Tanzania kuingia hatua ya nusu fainali ya mashindano ya klabu Aftika tangu mabadiliko ya muundo wa mashindano hayo mwaka 2017. What a story.

Heshima kwa Nasreddine Nabi. Top coach. Wakati Wanayanga wengi wakiwaza sherehe, Nabi aliwaza kufuzu na akaifanya timu icheze kwa namna ya kulinda ushindi wa mwanzo ugenini. Kwa nini?

Unavyoifungua timu na kushambulia mara kwa mara maana yake unatengeneza mazingira ya wapinzani kukuadhibu kwa mashambulizi ya kushtukiza na alifahamu fika kuwa Rivers United wanakuja wakiwa hawana cha kupoteza, sio kazi rahisi kucheza na timu ya namna hiyo.

Nusu fainali ni dhidi ya Amapiano sasa. Namuona kabisa Mwananchi akienda fainali labda aamue mwenyewe. Niagize ngapi Wanayanga tumalizie kivumbi na jasho? Namba yangu ileile.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: