Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezo wa Yanga vs Kaizer Chiefs kuoneshwa na DSTV

Kaiza Na Yanga Timu ya Kizer Chiefs wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Yanga

Sat, 22 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imefahamika kuwa mchezo wa Klabu ya Yanga dhidi ya Kaizer Chiefs utakaopigwa leo majira ya saa moja usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam hautarushwa na kituo cha Azam TV kwa Wananchi waliopo ndani ya mipaka ya Afrika ya Kusini.

Badala yake mchezo huo wa kuhitimisha Tamasha la "Siku ya Wananchi" utaoneshwa na DSTV na Azam Media wameridhia jambo hilo.

Ilikuwa ni kawaida miaka yote michezo ya Yanga katika kilele cha Tamasha la Siku ya Wananchi kurushwa na Azam TV pekee, lakini safari hii mambo ni tofauti na hasa ni kutokana na ujio wa timu ya Kaizer Chiefs.

Lakini kwa wakazi wa Tanzania na sehemu nyingine Duniani watauona mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa kupitia Azam TV.

Taarifa hiyo imetolewa na Klabu ya Yanga kama inavyosomeka kwa kirefu hapa chini;

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: