Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchele wa Kilombero wamfanya Manula ashindwe kwenda Ulaya

Manula One Aidhi Manula

Mon, 15 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa namba moja wa Klabu ya Simba na Timu ya taifa ya Tanzania, Aishi Salum Manula amesema kuwa ameshindwa kuondoka nchini kwenda kucheza nje ya nchi kutokana na mazingira anayohisi kuwa huenda yasiwe rafiki kwake.

Manula amesema hayo wakati akifanyiwa mahijiano maalum na mtangazaji Millard Ayo wakati akizungumzia maisha yake ya soka.

“Baada ya mkataba wa kwanza kumalizika Simba, nilipata ofa nyingi hapa nchini lakini bado Simba ilikuwa chaguo langu la kwanza. Hata hizo timu za nje zilikuwa bado zinanifanya niendelee kubaki Tanzania.

“Ninaamini mimi nacheza mpira ambao muda wangu hauwezi kuziki miaka 10 hadi 15, kwa hiyo nikifanya makosa kidogo tu, nitaharibu carrier yangu nzima na kunitoa kwenye mipango yangu, kwa hiyo lazima niwe makini sana sababu miaka hairudi nyuma na muda wa kurekebisha makosa unaweza ukaukosa.

“Moja ya mambo ambayo huwa sitaki kuchezea ni kipato. Nikipiga hesabu, maisha ninayoishi Bongo ni tofauti na nikiishi nje ya Tanzania. Kwa sasa naweza kuagiza mchele Kilombero ndio nakula kwangu, lakini nikitoka Tanzania maana yake ili niweze kupata chochote lazima niende supermarket, sasa gharama zinakuwa kubwa sana,” amesema Manula.

“Aidha, Manula amesema timu nyingi alizopata ni za Afrika Kusini lakini sio timu kubwa, kwa hiyo aliona anaweza kujiunga nazo halafu timu yenyewe haina uhakika wa kusalia hata kwenye ligi hivyo angepoteza malengo yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: