Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchambuzi: Wameshindwa kutafuta njia yao wanamuiga Manara

Ahmed Alyy Kamwe Ahmed Ally na Ally Kamwe

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: Tanzania

Vilabu vya Simba na Yanga kwa sasa vina wasemaji vijana ambao wamepewa dhamana ya kuvisemea vilabu hivyo vikubwa na vyenye historia kubwa nchini.

Mara kadhaa wasemaji wa Vilabu hivyo wamejikuta wakiingia matatani kutokana na kauli zao wanazotoa pindi wanapovisemea vilabu hivyo vyenye historia nchini.

Alianza Ally Kamwe ambae aishutumiwa kwa kutoa maneno ya kejeli kwa aliekuwa Kocha msaidizi wa Simba SC Juma Mgunda akimfananisha na andazi.

Hivi majuzi Msemaji wa Simba Ahmed Ally alisemekana kukashifu wachezaji wa Yanga kwa kauli zisizo za kiungwana.

Sasa mdau wa Soka ametoa ya moyoni akiwalenga wasemaji hao;

"Inasikitisha sana maafisa habari wa hivi vilabu wameshindwa kutafuta njia zao za kufanya promotion ya jambo fulani kwa timu zao mwisho wameishia kuiga yale aliyokuwa anayafanya Manara mbaya zaidi sasa hivi wametoka kwenye matani wanaenda mbali zaidi kugusa mtu binafsi hii ni mbaya sana

Sidhani kama Manara alikuwa anatumia njia hizi za kumu attach mtu moja kwa moja maisha yake yeye alikuwa anatumia nguvu kubwa kupromote jambo husika ila hawa maafisa habari wa sasa wao wanagusa maisha ya mtu binafsi

Kinachonisikitisha zaidi hawa wote walikuwa kwenye vituo vya habari na walikuwa wanampinga sana Manara kwa kauli zake laki wao sasa hivi ndo wamekuwa vinara wa hizo kauli ambazo wao walikuwa wanazikemea walipokuwa kwenye vituo vya habari"

Chanzo: Tanzania
Related Articles: