Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchambuzi: Walioathiriwa na refa sio Singida peke yao

Amina Kyando Amina Kyando.

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka kutoka Clouds Media, Farhan Kihamu amesema kuwa sio Singida Fountain Gate pekee walioathirika na maamuzi ya refa wa mchezo wa jana dhidi ya Simba SC.

Katika mchezo huo, mwamuzi Amina Kyando kutoka Morogoro ndiye alikuwa mwamuzi wa mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya sare ya bao 0-0 huku Simba wakisonga mbele katika hatua ya fainali kwa mikwaju ya penati 4-2.

Amina amekuwa gumzo mitandaoni hasa kutokana na kukataa bao la Singida FG dakika ya tano tu ya mchezo kwa tafsiri ya kwamba ilikuwa offside, jambo ambalo limewaibua wadau wengi wa michezo na mashabiki kuanza kuhoji uwezo wa refa huyo kuamua mechi ngumu kama ile.

"Sio Singida Fountain Gate pekee ambao wameathirika na maamuzi ya mwamuzi, nimeona mchezo ulikuwa umemzidi mwamuzi kwa pande zote mbili.

"Kuna maamuzi ambayo hakufanya kwa usahihi kwa pande zote mbili Singida Fountain Gate FC pamoja na Simba. Mchezo ungekuwa bora zaidi kama ungekutana na maamuzi bora kutoka kwa mwamuzi.

"Kwa hiyo kuna maamuzi ambayo yamewaumiza Singida na maamuzi mengine yameiumiza Simba," amesema Farhan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: