Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchambuzi: Pacome Zouzoua si wa kumtegemea

Pacome Zouzoua DF Pacome Zouzoua

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi maarufu wa soka nchini kupitia channel ya runinga ya TV3, Alex Ngereza amesema kuwa licha ya kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo wa jana dhidi ya KMC, kiungo mpya wa Yanga Sc, Pacôme Zouzoua si mchezaji wa kutegemea.

Zouzoua ambaye amesajiliwa na Yanga msimu huu akitokea ASEC Mimosas ya nchini Ivory Coast ameonyesha kiwango bora katika mechi alizocheza hasa ya jana huku akiisaidia timu yake kushinda bao 5-0 na yeye akiweka msumari wa mwisho.

"Pacôme Zouzoua alianza vibaya kwenye mchezo wake wa kwanza lakini leo ndio siku ya kutuonyesha uwezo wake. Ingawa kwangu mimi bado sioni kama anaweza kuwa mchezaji wa kutegemewa kwenye kikosi cha Yanga," amesema Alex Ngereza.

Yanga sasa inahesabu alama tatu na bao 5 ikiwa nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu baada ya kucheza mchezo mmoja tu ambao unaonyesha Yanga wamedhamiria kutetea taji lao kama ambavyo wamekuwa wakijinasibu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: