Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbrazil ampigia saluti Chama

Chama Clatous Name Mbrazil ampigia saluti Chama

Tue, 21 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuiongoza Simba kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Horoya juzi Jumamosi na kutinga robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Simba Mbrazil, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema anajivunia uwezo mkubwa ulioonyeshwa na mastaa wa timu hiyo hususani Clatous Chama na kuweka wazi sasa kazi ni moja tu, kutembeza vipigo.

Simba juzi Jumamosi ilifanikiwa kutinga hatua ya Robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kibabe baada ya kuibuka na ushindi mzito wa mabao 7-0 dhidi ya Horoya ushindi ambao uliwafanya wafikishe pointi tisa ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kati ya Vipers na Horoya.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kiungo Mzambia, Clatous Chama alikuwa kwenye kiwango kikubwa akifanikiwa kufunga mabao matatu na kutoa asisti moja.

Akizungumza nasi, Robertinho alisema: “Tumefurahi kuona tumepata nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali kwa kuwa ni malengo ambayo kama timu tuliyaweka wazi tangu mwanzo. Lakini kwa nafasi ya pekee nawapongeza wachezaji wangu hususani Chama kwa kucheza kwa kiwango kikubwa sana leo.

“Tunajua hatua tuna mchezo mgumu wa ugenini dhidi ya Raja Casablanca, lakini hatua ngumu ya robo fainali lakini naamini sasa tunazidi kuimarika na tunataka kucheza kwa kiwango hiki na kushinda mechi nyingi zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: