Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayeye: Sisi sio mashabiki, sherehe zimeisha

Mayele Caf.jpeg Mayeye: Sisi sio mashabiki, sherehe zimeisha

Fri, 12 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele amesema wanatamani kutangaza ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa kwenye dimba la Azam Complex Chamazi.

"Mechi hii imekuja katika kipindi ambacho tuna uchovu, mechi zimeongozana, lakini hiyo haitufanyi tushindwe kupambana na kupata alama tatu. Wachezaji tunajua umhimu wa mechi ya kesho, mashabiki wanajua umhimu wa mechi hiyo, sababu tukishinda tutatangazwa mabingwa wa msimu huu, kwa hiyo lazima tupambane.

"Sisi sio mashabiki, sherehe na furaha za ushindi wa juzi dhidi ya Marumo zimeshaisha, sherehe zinaendelea kwa mashabiki lakini sisi wachezaji tupo kwenye uwanja wa mazoezi kujiandaa na mchezo wa kesho, tunataka tushinde ili mechi zilisosalia tucheze tukiwa hatuna presha yoyote.

"Tutatumia nguvu nyingi sana kesho pamoja na maelekezo ya benchi la ufundi kuhakikisha tunapata ushindi," amesema Mayele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: