Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele naye ameomba kuondoka Yanga?

Fiston Kalala Mayele Life Fiston Mayele

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele ameomba kuondoka kwenye kikosi hicho na kwenda kutafuta changamoto nyingine huku klabu ya Kaizer Chief ikatajwa kumtaka Mkongomani huyo.

Taarifa ambayo tumeipata, nyota huyo ameonyesha dhamira ya kutoendelea kuitumikia klabu hiyo na anataka changamoto mpya.

Mmoja wa viongozi wa Yanga aliiambia Nipashe kuwa kwa sasa wanapambana kuhakikisha wanaendelea kupata huduma ya nyota huyo aliyechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio yao msimu huu.

“Viongozi wanapambana kuhakikisha Mayele anabaki, lakini mwenyewe ameomba kuondoka na ameuomba uongozi kukubali ofa yoyote itakayokuja kumuhusu yeye, kama viongozi tunatamani kuendelea kuwa na Mayele kikosini," alisema kiongozi huyo na kuongeza;

"Viongozi hatutakuwa na jinsi kama akibaki na msimamo wake kwa sababu tayari mchezaji ameshataka kuondoka huwezi kumzuia, lakini bado tunapambana kuhakikisha tunambakisha," alisema.

Aidha, alisema wapo wachezaji wengine ambao wameandika barua kuomba kuvunja mikataba yao ili waende wakatafute changamoto nyingine.

"Kuna wachezaji wengine wenyewe wameomba kuondoka, mazungumzo yanaendelea na mambo yatawekwa wazi siku si nyingi," alisema kiongozi huyo.

Wapambana kuwabakisha makocha Katika hatua nyingine, uongozi wa Yanga upo kwenye mazungumzo ya kuwabakisha makocha wake wasaidizi Helmy Gueldich na Khalil Ben Youssef.

Makocha hao mikataba yao imemalizika baada ya kuisha kwa msimu huu wa 2022/2023, kwa sasa wapo kwenye mazungumzo kwa ajili ya mikataba mipya.

“Mazungumzo yanaendelea, uongozi tumeamua kubaki na makocha hawa ambao watakuwa na msaada mkubwa na kocha mpya atakayeajiriwa hivi karibuni," alisema kiongozi huyo.

Alisema mbali na makocha hao, tayari mchakato wa kumpata kocha mkuu umeanza ambapo wamepokea zaidi ya maombi 100 ya makocha kuomba kazi ya kuifundisha timu hiyo.

"Kesho (leo) tutakaa na kupitia CV za makocha wote walioomba kazi, baada ya kujiridhisha tutamtangaza kocha wetu mpya atakayechukua nafasi ya Nabi (Nasreddine)," alisema.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema baada ya kutoa taarifa ya kuachana na Nabi, makocha wengi wametuma CV zao kutaka nafasi hiyo.

Alisema katika orodha ya makocha ambao wanaomba kazi hiyo, wapo makocha wakubwa ambao wanatamani kufanya kazi na Yanga.

“Binafsi sikutegemea kuona majina ya makocha wakubwa kama waliopo, baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC), Yanga imekuwa kubwa zaidi kila mmoja anatamani kufanya kazi katika klabu hii ya mafanikio, uongozi utapitia maombi yote na kuamua nani wa kumpa nafasi, mashabiki wasubiri tu,” alisema Kamwe.

Aidha, alisema watampa kazi kocha mwenye mafanikio ya soka la Afrika hasa yule ambaye amefanikiwa kutwaa taji lolote la CAF.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: