Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele goal Machine inayotetema kila kona

Mayele, Lomalisa Moloko Mayele goal Machine inayotetema kila kona

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Straika wa Yanga, Fiston Mayele 'Mzee wa Kutetema' amerejea nchini kutoka kwenye majukumu ya kimataifa akiiwakilisha timu ya DR Congo kwenye mchezo wa kufuzu fainali za Afrika (Afcon) 2023, iliyoifumua Gabon kwa mabao 2-0, huku akitupia moja na kutetema ugenini jijini Franceville.

Katika mchezo huo, Mayele aliwakimbiza mabeki wa Gabon na kuwapiga chenga kabla ya kufunga bao linalokaribia kufanana na lile alililoitungua Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu na kumpa tuzo ya Bao Bora la msimu kwenye tuzo za TFF za msimu wa 2022-2023.

Mayele alifunga bao hilo dakika ya 83 akitokea benchi kuchukua nafasi ya Yoane Wissa likiwa ni la pili kwenye mchezo huo baada ya awali Aaron Tshibola kuitanguliza dakika ya 34 na kufufumua matumaini ya DR Congo kwenda Ivory Coast ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Mauritani katika Kundi I.

Hilo sio jambo la kushtua kwa wanaomfuatilia Mayele, kwani mara nyingi amekuwa akifunga mabao katika nyakati zozote na mbele ya beki au kipa wa aina yeyote ile na kwa msimu huu amekuwa na zali aking'ara zaidi katika Ligi Kuu Bara, ASFC na Kombe la Shirikisho Afrika kiibuka Mfungaji Bora.

Staa huyo tayari amerudi Bongo kutokea DR Congo ambapo amekuja kukutana na viongozi wa Kwa sasa Yanga inapambana kutokana na kuwepo kwa dili la kutakiwa kwa mchezaji huyo na klabu kadhaa za Afrika na nje ya bara hilo, zikiwamo Esperence ya Tunisia na Zamaleck ya Misri.

REKODI ZINAMBEBA

Mayele alijiunga na Yanga msimu wa 2021/2022 akitokea AS Vita ya kwao DR Congo na tangu amefika kwa Wanajangwani hao amekuwa muhimiri wa safu ya ushambuliaji ya Yanga katika michuano yote huku akiwatungua makipa kibao.

Katika msimu wake wa kwanza akiwa na Yanga, Staa huyo anayesifika kwa staili yake ya 'Kutetema', alishika namba mbili kwenye vinara wa upachikaji wa mabao kwenye Ligi Kuu akifunga mabao 16, nyuma ya kinara George Mpole aliyeifungia Geita Gold mabao 17.

Hakuishia hapo, alifunga mabao mawili kwenye Kombe la Shirikisho la TFF (ASFC), na msimu huo huo alifunga bao moja kwenye mechi ya ngao ya jamii dhidi ya watani zao wa jadi Simba.

Kiufupi katika msimu wa 2021/2022, Mayele alifunga jumla ya mabao 19 katika Ligi Kuu, ASFC na Ngao ya jamii.

MSIMU BORA ZAIDI

Kwenye moja ya mahojiano aliyafanya na Mwanaspoti, Mayele alikiri msimu huu kuwa bora zaidi katika maisha yake ya soka.

"Kwakweli huu ndio msimu wangu bora zaidi, nimekuwa na kiwango bora na nimeweza kufikia malengo kwa asilimia kubwa," alisema Mayele.

Pamoja na yeye kusema hivyo lakini kauli yake inasapotiwa na namba zake katika michuano aliyoshiriki akiwa na Yanga.

Picha linaanza anakuwa mfungaji bora kwenye Ligi Kuu akifunga mabao 17 sawa na rafiki yake wa karibu Saidi Ntibanzokiza 'Saido' anayekiwasha Simba. Pia ndiye aliyewaa tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu sambama na Bao Bora mbali na kuwepo kwenye kikosi cha msimu cha Ligi Kuu 2022-2023.

Kisha akaisaidia Yanga kucheza fainali ya kombe la Shirikisho Afrika akaibuka mfungaji bora wa michuano hiyo akifunga jumla ya mabao saba akifuatiwa na Rango Chivaviro wa Marumo Gallants aliyefunga sita.

Ikumbukwe pia kabla ya kudondoka kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga ilianzia kwenye Ligi ya Mabingwa na huko Mayele alifunga mabao saba akipiga Hat trick mbili dhidi ya Zalan FC ya Sudan na bao moja dhidi ya Al Hilal katika sare ya mabao 1-1, nyumbani kwa Mkapa kabla ya kutolewa kwa kuchapwa 1-0 ugenini pale Omdurman, Sudan.

Pia aliitungia Simba mabao mawili kwenye mchezo wa ngao ya Jamii msimu huu mechi iliyomalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-1 na pia kwenye ASFC ambayo Yanga imeibuka bingwa alifunga mabao mawili.

Kiufupi msimu huu Mayele akiwa na Yanga amefunga jumla ya mabao 35, kwenye Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa Afrika, Kombe la Shirikisho Afrika, ASFC na Ngao ya Jamii.

Kwa maana hiyo katika misimu miwili ambayo Mayele amecheza Yanga amefunga jumla ya mabao 54 rekodi ambayo inambeba hadi leo na kufanya 'Wananchi', wahahe kumbakisha Jangwani kwani timu zenye uchumi mkubwa zaidi wa fedha zimeonyesha nia ya kumtaka licha ya kwamba bado ana mkataba wa mwaka mmoja na wakali hao wa Jangwani.

MBABE HAT TRICK

Mayele ndiye mchezaji aliyeongoza kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja 'hat trick' ukilinganisha na wakali wengine waliowika Bongo kwa msimu uliomalizika.

Mayele alifunga hat trick mbili dhidi ya Zalan FC katika Ligi ya Mabingwa Afrika na moja dhidi ya Singida Big Stars kwenye Ligi. 33 Jumla ya mabao aliyofunga Mayele katika Ligi Kuu Bara kwa misimu miwili mfululizo.

14 Mabao aliyofunga Mayele michuano ya CAF ikiwamo Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho 7 Idadi ya mataji aliyotwaa Mayele akiwa na Yanga, Ligi Kuu (2), ASFC (2), Ngao (2) na Mapinduzi.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: