Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele awashukuru Yanga, atoa neno kwa mashabiki

Mayele 4 Chrome Fiston Mayele

Sat, 24 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati akirejea nchini kutokea kwao DR Congo, mshambuliaji wa Yanga, Mkongomani Fiston Mayele ameibuka na kutamka kuwa tuzo tano alizozishinda msimu uliopita wa 2022/23 zimethibitisha ubora wake, huku akiwashukuru viongozi, wachezaji na mashabiki wa timu hiyo.

Mshambuliaji huyo amerejea nchini juzi Jumanne saa sita mchana akitokea DR Congo alipokwenda katika majukumu ya timu ya taifa hilo, iliyocheza dhidi ya Gabon katika mchezo wa kuwania kufuzu Afcon.

Tuzo hizo alizoshinda mshambuliaji huyo ni Mchezaji Bora, Mfungaji Bora, Bao Bora, Kikosi Bora cha msimu na Ufungaji Bora wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza nasi, Mayele alisema waliokuwa wanabeza ubora wake, umethibitishwa na tuzo hizo alizozibeba katika msimu uliopita ambao kwake ulikuwa na mafanikio makubwa.

Mayele alisema kuwa ubora wake haujatosha pekee, shukrani nyingi amezitoa kwa wachezaji wenzake waliompa ushirikiano wa kutosha uwanjani ikiwemo pasi nzuri za kufunga.

Aliongeza kuwa hajaridhirika na mafanikio mazuri aliyoyapata msimu huu, bado ana mengi ya kuyafanya katika msimu ujao kama akibakia kuendelea kuichezea timu hiyo.

“Tuzo ambazo nimeshinda katika msimu uliopita, zimethibitisha ubora wangu, na hilo lipo wazi kila mtu aliona jinsi nilivyoipambania timu yangu ya Yanga na kufanikiwa kushinda Tuzo.

“Niwashukuru viongozi, wachezaji wenzangu, mashabiki pamoja na benchi la ufundi ambalo lilihakikisha ninakuwa bora wakati wote kwa kuniandaa vema kabla ya mchezo.

“Bado sijafanikiwa na haya mafanikio ambayo nimeyapata, bado nina kibarua kigumu cha kupambana ili nipite zaidi ya mafanikio haya,” alisema Mayele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: