Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele atua nchini Nabi akisepa

Mayele Nabi Efdss Fiston Mayele na Nabi

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele ametua nchini leo Juni 20 akitokea kwenye majukumu ya timu ya taifa DR Congo.

Mayele alifunga bao katika ushindi wa DR Congo 2-0 ikiifunga Gabon ametua Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na mke wake na watoto wake.

Mayele akiwa nje ya jengo la abiria la 3 (terminal 3) alikutana na aliyekuwa kocha wake Yanga, Nasreddine Nabi ambaye anaondoka nchini leo.

"Safari njema profesa (Nabi)" ameandika Mayele kwenye ukurasa wake wa Instagram

Wawili hao walipiga picha ya pamoja nje wakati Mayele akiwa na tuzo zake ambazo alishinda msimu wa 2022/23 ikiwemo mchezaji bora Ligi Kuu, mfungaji bora (mabao 17 akifungana na Saido Ntibazonkiza) na bao bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: