Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele atoboa siri Yanga ilivyoipiga hesabu za Robo Fainali

Mayele227401 Mayele atoboa siri Yanga ilivyoipiga hesabu za Robo Fainali

Tue, 21 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Kalala Mayele amefunguka jinsi timu yake ilivyokuwa imepigia hesabu za kutoboa kwenye hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ili kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

Mayele ambaye ndiye kinara wa mabao katika klabu ya yanga, amefunguka hayo mara baada ya klabu hiyo kufanikiwa kutinga robo fainali kwa kuifunga Monastir ya Tunisia kwa bao 2-0 katika Dimba la Mkapa, juzi Jumapili, Machi 19, 2023.

“Sisi kama wachezaji na benchi la ufundi tuliweka malenngo yetu ya kushinda mechi zetu tatu za nyumbani, na tumefanikiwa pamoja na mashabiki wetu, mechi zote wametusapoti sana na tumefanya vizuri.

“Ile mechi ya ugenini pia ndiyo imetusaidia leo tumefuzu, ilikuwa mechi ngumu na presha ilikuwa kubwa, mvua zilikuwa kubwa na maji yalikuwa mengi, wachezaji walikuwa wakiteleza lakini tumepambana mwanzo mwisho na kupata matokeo mazuri.

“Nawashukuru sana mashabiki wetu wa Yanga, licha ya mvua kubwa tangu asubuhi mpaka jioni, lakini wamekuja wengi uwanjani, wameonyesha upendo na imetusaidia sisi wachezaji kupambana na kupata alama tatu, kiukweli nawapenda sana,” amesema Mayele.

Mpaka sasa, Mayele ana mabo matatu na assist moja katika mechi nne za hatua ya makundi ya mashindano hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: