Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele apewa zawadi Pyramids FC

Mayele Pyramids 7 Instagram Mayele apewa zawadi Pyramids FC

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fiston Kalala Mayele amepewa jezi namba 9 ndani ya kikosi cha Pyramids ikiwa ni ingizo jipya.

Nyota huyo msimu wa 2022/23 alikuwa ndani ya kikosi cha Yanga ambacho kilikuwa kinanolewa na Nasreddine Nabi.

Namba 9 inakuwa ni zawadi kwake Mayele kuendelea kuitumia kama alivyokuwa akifanya ndani ya Yanga na sasa atakuwa akiivaa mbele ya Waarabu hao wa Misri. Ni namba moja kwa utupiaji ndani ya Yanga msimu wa 2022/23 alipotupia mabao 17.

Mbali na kusepa na tuzo ya ufungaji bora alitwaa tuzo ya mchezaji bora na jina lake lilikuwa kwenye orodha ya kikosi bora.

Anaanza changamoto mpya ndani ya kikosi cha Pyramids akibainisha kuwa anakwenda kuanza changamoto mpya.

Mayele amesema anawashukuru Yanga na mashabiki kwa ajili ya sapoti ambayo wamempa ndani ya timu hiyo.

Ali Kamwe Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa mshambuliaji huyo watamkumbuka kutokana na kazi yake. “Mayele ni mshambuliaji mzuri tutamkumbuka kwa yote ambayo amefanya,” .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: