Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele amtengeneza mrithi wake Yanga

Mzize MAYELE Mayele amtengeneza mrithi wake Yanga

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kinda wa Yanga, Clement Mzize amemtaja mshambuliaji wa timu hiyo, Fiston Mayele ndiye anayemtumia kujifunza kupitie kwako jinsi ya kufunga mabao.

Kauli ya mshambuliaji huyo imekuja ikiwa ni siku chache atoke kufunga mabao mawili pekee katika ushindi wa mabao 4-1 walioupata hivi karibuni dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo huo ulikuwa wa hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports uliopigwa kwenye Uwanja wa SAzam Complex jijini Dar es Salaam.

Akizungumza nasi Jumatatu, Mzize alisema kuwa kwa muda mrefu alikuwa akitamani kucheza na Mayele, hivyo ndoto yake imetimia kwa kiasi kikubwa.

Mzize alisema kuwa bado anaendelea kujifunza kupitia kwa Mayele ambaye mara nyingi anampa ushauri ndani na nje mazoezi kwa lengo la kuhakikisha anakuwa bora.

Aliongeza kuwa anataka kuona ndani ya ndani ya msimu huu anafikia malengo yake kutegemewa katika kikosi hicho.

“Lipo wazi kwa hivi sasa katika ligi, Mayele ndio mshambuliaji bora mwenye uwezo mkubwa wa kufunga na kutengeneza nafasi.

“Hivyo ni lazima nijifunze kupitia yeye, kwani ana kiwango bora, ninaamini kupitia kwa kujifunza kwake ntakuwa bora zaidi.

“Mayele mara kadhaa amekuwa akinifundisha mengi ndani na nje Uwanja na nimekuwa nikifuata kile ambacho ananifundisha,” alisema Mzize.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: